Spika awaapisha Polepole na LulidaSPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo Novemba 30, 2020,  amewaapisha wabunge wawili walioteuliwa na Rais John Magufuli, ambao ni Humphrey Polepole na Bi Riziki Lulida kwenye viwanja vya bunge Dodoma.
Akiongea baada ya kuapishwa, Polepole amemshukuru Rais Magufuli na ameahidi kuwa sehemu ya Bunge itakayoleta maendeleo kwa umma.

Kwa upande wake Lulida amemshukuru  Magufuli  kwa imani yake kwake na amehaidi kutomwangusha.

“Nitafanya kazi kwa moyo wangu wote, sitamuangusha, nipo hapa kama mbunge niliyeapishwa; sina mengi, nawashukuru wananchi wa Lindi na Watanzania kwa maombi yao,” alisema Lulida.

Wabunge hao wameapishwa baada ya kuteuliwa jana Novemba 29 na Magufuli kuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

  1. Hongereni Waapishwa. you deserve .

    MSITUANGUSHE, IMANI MLIOPEWA NI DENI KUBWA.

    KACHAPENI KAZI, KWELI KWELI.

    ReplyDelete