Sven: Hii Ndiyo Simba Ninayoitaka
BAADA ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Coastal Union na kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa, Kocha wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, ameibuka na kusema kuwa timu yake ilifuata maelekezo kwa asilimia kubwa, ndiyo maana waliibuka na ushindi mnono.

 

Simba, licha ya kuibuka na ushindi huo mnono, bado inabakia katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, mara baada ya kufikisha pointi pointi 23.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Sven alisema kuwa siri kubwa ya ushindi huo ni wachezaji wake kufuata maelekezo yake na kutambua majukumu yao uwanjani, jambo ambalo amelifurahia kwani ndio jambo ambalo analipenda lifanyike mara kwa mara.

 

“Wachezaji wengi walicheza kufuata maelekezo niliyowapa, wengi walitimiza majukumu yao kama nilivyowaagiza, mabeki walikaba ipasavyo na kule mbele wachezaji walitengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao na mabao yakapatikana.

 

“Hiyo ndiyo siri ya ushindi, lazima kama kocha wachezaji wacheze kulingana na maelekezo ya mwalimu, nimefurahi kwa ushindi huu, naamini tunahitaji kushinda mechi nyingi zinazofuata mbele yetu ili tuweze kufikia malengo yetu,” alisema kocha huyo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments