Taharuki ya covid-19 nchini China
Hali ya taharuki imetanda kwenye uwanja wa ndege baada ya wafanyakazi wawili kukutwa na virusi vya corona (Covid-19) katika mji wa Shanghai nchini China.

Wafanyakazi wawili wanaohudumu kwenye uwanja wa ndege wa Shanghai nchini China walikutwa na virusi vya corona (covid-19).

Kufuatia hali hiyo, wasimamizi wa uwanja wa ndege walichukuwa uamuzi wa kuwapima wafanyakazi wote na kusababisha hali ya mvutano na mkanyagano.

Maelfu ya wafanyakazi waliokwenda kupima covid-19 walisababisha msongamano na kukanyagana.

Wengi wao walionekana kuanguka na kupoteza fahamu kwenye msongamano uliotokea.

Hadi kufikia sasa watu zaidi ya 12,000 wameweza kupimwa katika shughuli hiyo ya upimaji iliyoanza usiku na wote hawakukutwa na virusi.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments