Taifa Stars Yafufua Matumaini ya Kufuzu AFCON


Kiungo machachari Feisal Salum 'Fei Toto' aliinusuru timu ya Taifa ya Tanzania' Taifa Stars' kupokea kipigo kutoka kwa Tunisia katika mechi ya marudiano ambayo ni ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Africa 'AFCON' zitakazochezwa mwakani nchini Cameroon.

Faisal aliyetokea benchi akichukua nafasi ya Himid Mao dakika ya 36, aliisawazishia Stars dakika ya 47 kufuatia pasi ya John Bocco ambaye alimtulizia mpira wa krosi ya Ditram Nchimbi ambaye alifanya kazi nzuri kabla ya bao hilo kufungwa.

Tunisia ambao alama moja imewahakikishia tiketi ya kucheza michuano ya AFCON mwakani, lilifungwa na Saif Akhoui dakika ya dakika ya 11 ya mchezo.


Matokeo hayo yanaiilazimu Taifa Stars kushinda mechi mbili dhidi ya Equatorial Guinea na Libya ili kujihakikishia nafasi moja iliyosalia kufuzu michuano hiyo mikubwa ya Afrika.


Tunisia imeungana na mataifa ya Senegal, Algeria na Cameroon ambazo zilikata tiketi mapema baada ya michezo yao iliyopigwa hivi karibuni wakifanikiwa kukusanya alama za kutosha.


Stars ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 4, wakati nafasi ya pili ikishikiliwa na Equatorial Guinea wenye alama 6 nao Libya wakiburuza mkia katika kundi J wakiwa na alama 3

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments