Tanzia: Kamanda Kidavashari Afariki DuniaNAIBU Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Zahir Kidavashari,  amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne, Novemba 17, 2020 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya DCMC Ntyuka jijini Dodoma.


Kidavashari aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.


Akizungumza na Global Digital, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, SACP Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa msiba huo.


“Taarifa za msiba huo ni za kweli, Kidavashari amefariki dunia.” 


Taarifa zaidi tutakueleta…. 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE