Tommy Flavour afunguka kuhusu kumchora Tattoo Lyyn

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Msanii wa Kings Music Records Tommy Flavour, amesema tattoo zilizopo mwilini mwake ni za muda mrefu na wala hajawahi kuchora tattoo yenye jina au sura ya mpenzi wake Official Lyyn.

Tommy Flavour amesema hatarajii kuchora tattoo ya mpenzi wake huyo kwa sababu hataki kujutia baadaye pia haamini kwamba kumchora mtu ndiyo atakuwa ameonyesha upendo kwake. 


"Sijawahi kuchora tattoo yenye jina lake wala sura yake na hata yeye hajanichora, tattoo ambazo nipo nazo ni za muda mrefu japo kuchora ni maamuzi yako mwenyewe, unaweza ukachora halafu baadaye ukajuta na mimi sitaki kufikia kwenye hali hiyo, sisemi hivi kama nitaachana naye au kuna lolote baya litatokea ila siamini kama nikifanya hivyo ndiyo nitakuwa naonyesha mapenzi kwake" ameeleza Tommy Flavour

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad