11/01/2020

Tommy Flavour wa Alikiba akata mzizi wa fitnaMsanii wa lebo ya Kings Music ya Alikiba Tommy Flavour amesema hataki kufananishwa na wasanii wengine ambao wapo kwenye menejmenti zingine kwa sababu kila mtu ana mikakati yake kwenye suala zima la kufanya kazi.


Tommy Flavour amesema 'promotions' wanazofanyiwa wasanii wengine kwenye lebo zao wala hata hazimshuti ila anachoamini ni uwezo na kipaji cha mtu ndiyo kitamfanya awe juu kuliko kutumia nguvu ya 'promotions'.


"Hata kama unam-promote vipi msanii ila uwezo na kipaji chake ndiyo kitambeba na ndiyo itamfanya aendelee kwenye muziki, mimi naamini nitafika mbali na menejmenti yangu itanifikishia hilo, hata walivyonisaini haikuwa kwa ajili ya kunishindinisha na wasanii wengine kutoka lebo zingine" amesema Tommy Flavour 

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger