11/20/2020

Tonombe Aeleza Ishu ya Kwenda Simba
KIUNGO wa kimataifa wa Congo anayekipiga Yanga, Mukoko Tonombe, amesema anaipenda sana Yanga hivyo hawezi kuondoka kwa sasa.

 

 

Hiyo ni baada ya kuzagaa tetesi za kiungo huyo kutua kuichezea Simba katika usajili wa dirisha dogo baada ya Wekundu hao kupata taarifa za kuwa kiungo huyo amesaini mkataba wa miezi sita Jangwani.

 

 

Ameyasema hayo kupitia Instagram akiwa ‘live’ huku akitumia Lugha ya Kiswahili ambayo inaonekana bado hajaifahamu vizuri kwa kusema; “Naipenda sana Yanga mimi, Simba hapana kabisa, sina mpango nao, lakini pia naitakia kila la kheri timu ya taifa, Taifa Stars.”

 

 

Tonombe alisema kuwa anaamini Tanzania itashinda kuanzia bao mbili dhidi ya Tunisia huku akimtabiria kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ kufunga bao katika mchezo huo ambao ulichezwa usiku wa kuamkia juzi.

 

 

Stars jana ilishuka uwanjani saa nne usiku Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuvaana na Tunisia katika mchezo wa kuwania kufuzu Afcon.

 

 

Habari hii inaonekana kuwakata maini Simba ambao walikuwa wanaamini kuwa wanaweza kumshawishi kiungo huyo mwenye mabao mawili kwenye ligi na tuzo moja ya mchezaji bora wa mwezi.

 

Mbali na tuzo hiyo, pia ana tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki Yanga ambayo ameipata mara mbili pamoja na ile ya mechi ya Simba na Yanga iliyopigwa hivi karibuni.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger