Tume ya uchaguzi Uganda yawataka polisi kutowazuwia wagombea urais

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Tume ya uchaguzi nchini Uganda imewatahadharisha polisi nchini humo dhidi ya kuwazuia wagombea wa urais kuendesha kampeni zao.
Tume hiyo imesema kuwa imepokea baadhi ya malalamiko kutoka kwa wagombea wa urais na pia kuona taarifa zavyombo vya habari kwamba polisi inazuia na kuvuruga kampeni zao .

Wakati huo huo katika taarifa ya pamoja ya mabalozi wa nchi za Muungano wa Ulaya nchini humo, wameeleza kutofurahishwa kwao na ghasia zilizotawala kampeni ya uchaguzi tarehe 18 na 19, Novemba nchini humo.

Wamesema Uganda ilishuhudia ghasia na maandamano pamoja na matumizi yasiyofaa ya vikosi vya usalama dhidi ya raia na kuvitaka vyama vyote vya kisiasa na wagombea wake kuwataka wafuasi wao kuacha ghasia na matumizi ya lugha mbaya.

Wametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kumaliza uchokozi unaolenga kuleta ghasia au kusababisha ukiukaji wa sheria.

Hii inajiri huku Kiongozi wa upinzani nchini huo Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine alilalamikia kuzuiwa kuendesha kampeni zake katika mji wa Hoima magharibi mwa nchi hiyo.

Katika ujumbe wake wa twitter Bobi Wine amesema kuwa polis walifunga barabara za kuelekea katika mji huo ili kumzuwia kufika katika hoteli aliyotarajia kupata malazi na kuziamuru hoteli zaote katika mji huo zisimpokee na timu yake, na hivyo kuwalazimisha kulala ndani ya magari:


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad