Tuzo ya AFRIMMA niliyopata imenipa ari ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii - ZuchuMsanii wa Kizazi kipya Bongo Fleva Zuhura Othman maarufu ZUCHU kutoka lebo ya muziki ya WASAFI amesema tuzo aliyojishindia ya AFRIMMA ni kielelezo tosha kwamba Muziki wake unatazamwa ulimwenguni hivyo kuwaomba Watanzania kuendelea kumuunga mkono katika kazi zake.

Akizunguza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ZUCHU amesema Watanzania wanamchango mkubwa katika mafanikio yake hivyo kuwaomba kuendelea kuifuatilia kazi zake.


"Tuzo ya AFRIMMA niliyopata imenipa ari ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili nifike mbali zaidi na hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Muziki wangu unatazamwa ulimwenguni"Amesema ZUCHU.


Pia amewahasa watoto wa kike wanaochipukia kama kimuziki wasikate tamaa bali waendelee kupambana ili siku moja waone matunda ya kazi zao.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE