Twaha Kiduku "Mwakinyo ni bondia bora ila asije akalewa sifa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Bondia Twaha Kiduku ameeleza kuukubali uwezo wa Hassan Mwakinyo na kumtaja kuwa ni bondia bora ila akamtahadharisha asije akalewa sifa kwa mafanikio anayopitia sasa ulingoni.

Twaha bondia namba mbili kwa ubora nchini kwenye uzani wa super welter nyuma ya Mwakinyo amempongeza mpinzani wake huyo kwa uwezo aliouonyesha hivi karibuni alipotetea ubingwa wa Mabara wa WBF kwa ushindi wa TKO dhidi ya Jose Carlos Paz wa Argentina.


"Ni pambano ambalo Mwakinyo alicheza vizuri mno, kuanzia raundi ya kwanza hadi ya nne aliposhinda. Nilikuwa ukumbini na kushuhudia na nilikwenda kumpongeza kwa namna alivyocheza.


"Nilitamani kumpa ushauri huu, lakini mazingira hayakuwa rafiki pale, nimsisitize tu mdogo wangu na bondia mwenzangu kuendelea kukaza afanye vizuri zaidi ya anavyofanya sasa. Isije ikatokea akalewa sifa atapotea," alisema #Twaha anayemzidi Mwakinyo miaka mitatu akiwaambia Waandishi wa Habari.


Akaongeza, "Mwakinyo namuamini hana masihara na mazoezi, ninachoweza kumwambia aendelee kukaza hivyo hivyo ili azidi kufanya vizuri na kuitangaza 'boxing' ya Tanzania kimataifa kama walivyofanya waliomtangulia na mabondia wengine wanaopigana sasa nikiwamo mimi," amesema.


Kuhusu kuwa na ndoto za kuzichapa na bondia huyo, #Kiduku amesisitiza kuwa bado mpango huo upo na unacheleweshwa na #Mwakinyo mwenyewe.


"Natamani itokee akubali kupigana na mimi, ila naamini ipo siku itatokea tu na pambano kati yangu na Mwakinyo litapigwa," amesisitiza.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad