Ubinadamu Umeenda Wapi Jamani..Wanakijiji Wadaiwa Kukatwa Vichwa Msumbiji

 


TAARIFA kutoka Msumbiji zinasema kuwa wanamgambo wa Kiislamu wamevamia vijiji Kaskazini mwa eneo la Muidumbe mkoa wa Cabo Delgado, Jumamosi na Jumapili.

 

Vyombo vya habari vya eneo vimesema kuwa wanakijiji walikatwa vichwa na mali zao kuharibiwa. Msemaji polisi wa eneo alikanusha madai kuwa kuna wanavijiji ambao bado wanashikiliwa na wanamgambo wa jihadi.

 

Kundi hilo la wanamgambo ambao wenyeji wanalifamau kama al-Shabab, limekuwa likidhibiti maeneo ya msingi ya kaskazini mwa Mocímboa da Praia tangu mwezi Agosti.

 

Pia, zaidi ya watu 1,500 wameuawa huku theluthi moja ya watu wakilazimika kuhama makazi yao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.


CREDIT: BBC SWAHILI

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE