Uchebe Atoa Kauli ya Kibabe kwa Mwanamke wake mpya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Aliyekuwa mume wa msanii Shilole, mfanyabiashara Uchebe amejibu mapigo kwa wanaoleta maneno kuhusu mpenzi wake mpya aitwaye Official Agness, kwa kusema sasa hivi yeye sio mume wa mtu na hayupo kwenye ndoa hivyo anaweza kuchukua mwanamke yeyote anayemtaka.

 Uchebe amesema kila mtu aangalie maisha yake na watu wasimjaji sana kwani hata yeye ana 'protocal' binafsi za maisha yake.


"Sipo kwenye ndoa na sasa hivi mimi sio mume wa mtu, nina uwezo wa kutoka na yeyote na kufanya chochote kama mwanaume, na mwanaume lazima amfuate mwanamke ili kujua anataka nini haijalishi awe muislam au muikristo" amesema Uchebe


Aidha ameongeza kusema "Maisha yapo tofauti wasijaji sana kuhusu mimi waangalie maisha yao yanaenda vipi, mimi pia nina protocal zangu kwa mwanamke kwanza awe anafanya ibada na asinywe pombe maana siwezi kukaa na mwanamke mlevi kwangu".

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad