Uchebe wa Simba Atupiwa Virago Black Leopards

 


Klabu ya Black Leopards ya Afrika ya Kusini imevunja mkataba na aliyekuwa kocha wa zamani wa klabu ya Simba ya Tanzania Mbelgiji Patrick Aussems.

Aussems alijiunga na Leopards mwezi uliopita mwaka huu na kusaini mtababa wa miaka mitatu lakini ameondoka baada ya mwezi mmoja kupita.


Inaelezwa kwamba matokeo mabovu ya timu hiyo ya timu hiyo kwenye ligi pamoja na kutokuwa na maelewano mazuri na uongozi ni sababu zilizopelekea yeye kuachana na wababe hao kutoka jimbo la Limpopo.


Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Simba ya Tanzania, aliiongoza Black Leopards kwenye michezo mitatu ya ligi na kupteza yote huku wakishika mkia kwenye msimamo wa ligi kuu nchini humo.


Leopards waliachana na Aussems tangu jumapili wili iliyopita na jana jumatatu hakuwa sehemu ya mazoezi ya timu hiyo.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE