Ujerumani Yaipa Barabara Jina la Waziri Mwanamke Tanzania

 


MADIWANI katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, wamepiga kura ya kuondoa jina la barabara moja alilopatiwa kwa heshima gavana mmoja wa nyakati za ukoloni katika  Afrika Mashariki, aliyeshutumiwa kwa mauaji na kuweka jina la mmoja wa wanaharakati wa kupigania uhuru nchini Tanzania, Lucy Lameck.

Lucy alikuwa waziri wa kwanza mwanamke kwenye Wizara ya Ushirika na Maendeleo  pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi maarufu katika vuguvugu lililopigania uhuru.  Barabara ya Wissmannstra├če, ambayo ilipewa jina la Hermann von Wissmann, sasa itaitwa Lucy-Lameck-Stra├če.

Von Wissman alikuwa Gavana wa Taifa la Ujerumani Afrika Mashariki ambayo kwa sasa ndiyo mataifa ya Tanzania , Burundi na Rwanda  mwishoni  mwa karne ya 19 na kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Der Tagesspiegel  anadaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya wananchi wengi.

 

Taarifa ilisema kwamba kampeni hiyo ilikomesha kuheshimiwa kwa ”Von Wissmann na nafasi yake  kuchukuliwa na mwanamke Mtanzania ambaye alipinga ukoloni na ubaguzi wa rangi”.

Iliongeza kwamba Wissmann alikuwa mbaguzi na mhalifu wa kivita.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments