Ukatili wa Kijinsia Wachukua Sura Mpya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Mwanaharakati, kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC), Joram Bwire, amesema kuwa yapo mambo madogo madogo ambayo inabidi yafanyiwe kazi ili kutomekeza ukatili wa kijinsia ikiwemo maboresho ya kamati zilizoundwa.


Akizungumza katika kipindi cha Supa breakfast, cha East Africa Radio, Joram Bwire amesema licha ya ukatili wa kijinsia kuonekana unazidi kushika kasi serikali imefanya juhudi mbalimbali kuhakikisha inaondoa tatizo hilo.


“Kuna mambo madogo madogo inabidi yafanyike kwamba hizi kamati inabidi ziboreshwe kwa kujengewa uwezo ili kurahisisha utendaji kazi” amesema


Aidha Bwire akizungumzia ukatili wa ukeketaji amesema kuwa katika kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa lazima chanzo chake kijulikane ili liweze kutatauliwa huku akisema kuwa  tatizo hili limechukua sura mpya ambapo watoto ufanyiwa ukeketaji mara tu wanapozaliwa hospitalini hivyo kuwalazimu kuweka ulinzi shirikishi hospitalini kwa ajili ya kudhibiti tatizo hilo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad