11/13/2020

United Waanza Kuhofia Tabia ya Greenwood

 


TIMU ya Manchester United imepata hofu kuhusiana na tabia ya kinda wao Mason Greenwood. Klabu hiyo imesema kuwa kuna hofu kubwa kuwa mchezaji huyo amekuwa akibadilika tabia kila siku na sasa hapati muda wa kutosha wa kulala.

 

Inaelezwa kuwa kinda huyo ni mtoto wa bata sana hali ambayo inamyima nafasi ya kutosha kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu England. Hivi karibuni imekuwa ikiripotiwa kuwa staa huyo amekuwa akishindwa kufanya vizuri mazoezini.

 

Hata hivyo, habari zinasema kuwa kocha wa timu hiyo Ole Gunnar Solkjaer, amesema kuwa anataka kupambana naye ili arudi kwenye kasi yake. Ameanza kuwa na tabia mbovu kuanzia alipoondolewa kwenye kambi ya timu ya taifa ya England kutokana na kumuingiza mwanamke kwenye vyumba vya kambi ya taifa.


MANCHESTER, England

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger