Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Ureno Wautema Ubingwa wa Uefa Nations League

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURETIMU ya Taifa ya Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kutinga kwenye Fainali za UEFA Nations League ambazo ( zile timu 4 za mwisho ) baada ya kuibuka kidedea dhidi ya bingwa mtetezi Ureno kwa bao 1-0.


 


Ufaransa wanaongoza kundi C kwa pointi 13, goli pekee katika mechi ya jana usiku lilifungwa  na kiungo N’golo Kante dakika ya 53. mechi ilikuwa ya kulipiza kisasi kwa ufaransa ambao walipoteza kwenye fainali ya Euro mwaka 2016 katika uwanja wao wa nyumbani.
 


Sasa ni rasmi Ronaldo na vijana wake wamelitema kombe na kutakuwa na bingwa mpya hapo mwakani . Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kushindwa kufunga katika mechi zote 6 dhidi ya Ufaransa ndio timu pekee amecheza mechi nyingi za kimataifa bila kuifunga.


Ufaransa walicheza bila ya mshambuliaji wao tegemeo Kylian Mbappé ambaye ni majeruhi.

Post a Comment

0 Comments