Uteuzi wa wabunge viti maalum CHADEMA ulifuata sheria- Prof Kilangi
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Profesa Adelardus Kilangi amewaonya CHADEMA kutowabugudhi wabunge wa chama hicho wa viti maalum kutoka chama hicho.
Profesa Kilangi amesema, mchakato wa Wabunge wa viti Maalum kutoka CHADEMA umefuata Sheria na Katiba, hivyo hawapaswi kubugudhiwa.

Awali Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai alisema, kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda Wabunge walio wachache na maslahi yao na kuahidi kufanya hivyo kwa nguvu zake zote,

Kuhusu Wabunge 19 wa viti Maalum kutoka CHADEMA Bw Ndungai alisema wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu.Amesema majina ya wabunge wa viti maalum alipewa na na Tume ya Uchaguzi, na kazi yake ni kuwaapisha Wabunge hao na ameshafanya hivyo.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

 1. Hili ni Dhahiri kuwa yule wa kule nje
  hakupenda kuona minyika amesha peleka
  Wateuuliwa, ndiyo akaanzisha magenge ndani huku akijua fika ile justification yake ya kumwaga Damu haitokuwa na Mashiko. Minyika yuko njia ya dilemma .

  Kina mama Oyeee.
  Tufikirie Takrim yao 2025 tunzo depends on their performance ktk kulitumikia taifa.

  ReplyDelete