‘Vita’ ya Biden na Trump Yazidi Kukolea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden amelaani kitendo cha, Donald Trump kutokukubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais na kwamba amekuwa akituma ujumbe mbaya sana kuhusu Marekani.

Biden amesema, alikuwa na uhakika kuwa, Trump alikuwa anajua kuwa asingeshinda na kila kitu kilionekana wazi, kwa kuwa alikuwa hajitumi kabisa katika majukumu yake.

Biden alikuwa akiongea katika mkutano wa simu na Magavana, wakiwemo wa Democrats na Republicans, kuhusu janga la corona.

Alihojiwa kuhusu suala la Trump kutokubali ushindi wake, Biden amesema rais anatuma ujumbe wa kutisha kwa dunia nzima kuhusu jinsi demokrasia inavyofanya kazi na hilo anapaswa kulikumbuka kwa kuwa amekuwa rais ambaye hawajibiki katika historia ya Marekani.

Kulikuwa na marudio ya kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika Jimbo la Georgi, na Biden alipata ushindi katika jimbo hilo, Trump alifungua kesi ya madai ya wizi wa kura. Madai yake yote ya kisheria yaligonga mwamba na kushindwa kufanya mabadiliko yoyote.


 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad