Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Waangalizi wa kimataifa: madai ya Trump hayana msingi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMkuu wa ujumbe wa waangalizi wa kimataifa kwenye uchaguzi wa Marekani amesema jana kwamba madai ya Rais Donald Trump hayana msingi, yanayosema kwamba kumefanyika udanganyifu katika uchaguzi huo. 


Michael Georg Link anayeongoza ujumbe wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya, OSCE ameongeza kuwa madai ya Trump yanadhoofisha imani ya umma kwa taasisi za kidemokrasia nchini humo. 


Katika ripoti ya awali, ujumbe huo pia ulionya kwamba matamshi ya Trump wakati wa kampeni zake, yaliangaliwa na wengi kuwa na uwezo wa kuchochea vurugu za kisiasa baada ya uchaguzi. Ujumbe huo pia ulitaka kuhesabiwa tena kwa kura zote baada ya timu ya kampeni ya Trump kusema kwamba imefungua mashtaka mahakamani ya kusitisha mchakato huo katika majimbo muhimu ya Michigan na Pennsylvania.

Post a Comment

1 Comments

  1. Wafa Maji, wapo wengi.
    kutapa tapa ni hulka yao ulimwengu mzima. siyo kiguru tu.

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)