11/07/2020

Wachimbaji Wajeruhiwa kwa Mapanga, VisuWACHIMBAJI wadogo wanane wajeruhiwa kwa silaha za jadi yakiwamo mapanga, visu sehemu mbalimbali za miili yao katika machimbo ya dhahabu ya Irasanilo, Buhemba, yaliyopo wilayani Butiama mkoani Mara chanzo kikiwa ni kugombania maduara ya uchimbaji.


Baadhi ya majeruhi hao wamesema wakiwa wanaendelea na uchimbaji ndani ya mashimo, walivamiwa na kundi la watu ambao walianza kuwashambulia kwa nondo, mawe na kuwachoma na visu sehemu mbalimbali za miili.


Akizungumzia tukio hilo mmiliki na katibu wa duara hilo namba tisa (A), Mwajuma Seif amesema kabla ya tukio hilo duara hilo lilikuwa na mgogoro huku uongozi wa wachimbaji hao wadogo mkoani Mara, wakatoa tamko la kulaani tukio hilo la kikatili kwa wenzao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger