google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Wakurugenzi Wawili Kizimbani Kwa Makosa 45 Yakiwemo Ya Utakatishaji wa Sh Bil 1.6 | UDAKU SPECIAL

Wakurugenzi Wawili Kizimbani Kwa Makosa 45 Yakiwemo Ya Utakatishaji wa Sh Bil 1.6

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wakurugenzi wawili wa Kampuni ya Vinywaji Vikali (BEVCO) akiwemo Raia wa Ufaransa, Melaine Philippe wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa 45 ikiwemo utakatishaji fedha wa Sh.Bil 1.6.


Washitakiwa hao ambao wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi namba 87 ya mwaka 2020 wamefikishwa mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  na kusomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.


Washitakiwa hao wamesomewa  mashitaka yao na Wakili wa Serikali, Magela Ndimbo ambapo amedai walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti ambapo wana makosa ya Kughushi, Kukwepa Kodi, Kuwasilisha Nyaraka za Uongo, Kuisababishia hasara TRA na Utakatishaji fedha.


Kosa la utakatishaji fedha wanadaiwa kulitenda kati ya Oktoba 31, 2017 na June 2020 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam ambapo wanadaiwa walimsaidia Samson Rwegasira na Thierry Lefeuvre kujipatia Sh.Bil 1.6 wakati wakijua fedha hizo zinatokana na  makosa ya kukwepa kodi, kughushi.


Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Ndimbo amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo anaomba kesi hiyo ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.


Washitakiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo washtakiwa wamerudishwa rumande na kesi imeahirishwa hadi Desemba 3, 2020.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad