11/11/2020

Wanafunzi watumia mitumbwi kwenda shule, Geita



Wanafunzi wa Kisiwa cha Izumacheki kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Geita, mkoani Geita, wanalazimika kuvuka maji kwa kutumia mitumbwi inayosafiri kwa muda wa nusu saa kwenda shuleni, Kata ya Nkome, kutokana na eneo wanaloishi kutokuwa na Shule, kitendo kinachohatarisha usalama wao.



Baadhi ya wananchi wakipanda mtumbwi.

Kuangalia video bofya HAPA

Hali ya ukosefu wa shule ya sekondari katika kisiwa hicho, imesababisha mkuu wa wilaya ya Geita, Fadhili Juma, kutembelea katika maeneo hayo na kuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuweka mikakati ya ujenzi wa shule ya sekondari, ili kuondoa changamoto inayowakabili wanafunzi hao.


“Halmashauri yangu ninaiagiza ianze mpango wa ujenzi wa sekondari, kwa sababu ni ‘risk’ kwa watoto kupanda boti kila siku kwenda kutafuta elimu kwenye Kata jirani na mpango wa serikali hii ni kuwa na sekondari katika kila Kata”, amesema DC Juma.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

1 comment:

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger