Wananchi watakiwa kuimalisha Usafi na Ulinzi wa mtoto kuepuka kupata magonjwa ya Milipuko

Na Baraka Messa, Mbozi.
WANANCHI Wilayani Mbozi mkoani Songwe wametakiwa kuimalisha usafi msimu huu wa mvua ili kuwaepudha watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano kudhurika na magonjwa mbalimbali ya milipuko kutokana kupenda kutumia baadhi ya vifaa vilivyo tupwa pamoja na kupenda kuchezea maji machafu.

Hayo yametolewa na Kaimu Afisa afya Wilaya ya Mbozi Togolai Gembe Wakati akiongea na mwandishi wa gazeti hili kuhusiana na jitihada zinazofanyika kuhakikisha watoto wa dogo chini ya miaka mitano wanakuwa salama kutokana na agizo la mkuu wa Wilaya hiyo John Palingo kuwataka viongozi wa afya ngazi ya Wilaya, Kata na vijiji kuhakikisha wanatoa elimu kuhusiana na utupaji wa barakoa na baadhi ya vifaa vilivyotumika na watu wazima  ambavyo ni hatari kusababisha magonjwa ya kuambukiza na milipuko.

Gembe alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kutoa elimu kwa wananchi katika kata zote za Wilaya ya Mbozi kuhakikisha wananchi na watoto wadogo hasa chini ya miaka mitano wanakuwa salama muda wote hasa kipindi hiki Cha mvua ambacho huwa kina kuwa na magonjwa mengi hasa ya matumboambayo husababishwa na uchafu.

Alisema kwa Wilaya ya Mbozi baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwa bizee na shughuli zao za uzalishaji na kuwasahau watoto wakicheza katika mazingira hatarishi huku wakitumia baadhi ya vifaa vilivyotumika kama vile mipira ya kondom iliyotumika, nepi za watoto zilizizotumika, taulo za kike zilizotumika pamoja na barakoa kipindi cha korona.

“Nitumie nafasi hii kuwakumbusha tena wananchi wa Wilaya ya Mbozi kuzingatia usafi , kwa kuhakikisha vifaa kama taulo za kike, nepi za watoto na barakoa kutupwa sehemu husika na kuchomwa moto ilii kumnusuru mtoto ndogo kupata madhara ,

Sheria zipo wazi hatutasita kuwachukulia hatua wale wote ambao watashindwa kuzingatia usafi hasa kipindi hiki Cha mvua ambacho kina hitaji usafi wa Hali ya juu kuepuka magonjwa ya milipuko kama vile kipindu pindu na magonjwa ya tumbo” alisema Gembe.

Aliongeza kuwa  kipindi cha mvua kinahitaji usafi na ulinzi mzuri wa watoto kwa sababu watoto hupenda kuchezea maji machafu ambayo huhatarisha afya za watoto kwa kuweza kusombwa na maji na kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya matumbo.

Hivi karibuni mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo akiongea na mwandishi wa gazeti hili aliwataka watalaamu wa afya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya kutupa ovyo taka taka na baadhi ya vifaa vilivyotumika vinavyopelekea watoto kuwa kwenye hatari kubwa ya kupata madhara ya kupata magonjwa ya Milipuko na magonjwa ya kuambukiza kwa watoto.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments