11/03/2020

Wanaodaiwa kutaka kuchoma moto nyumba ya Katambi wakamatwa
Polisi Mkoani Shinyanga imewakamata watu tisa kwa tuhuma za kutaka kuchoma moto nyumba ya Mbunge Mteule wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi kupitia CCM.

Miongoni mwa watuhumiwa ni aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CHADEMA, Salome Makamba, ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana.


Watuhumiwa wengine ni wanaume nane wanaoendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika, watawafikisha Mahakamani.


Watuhumiwa waliposhawasha moto, Katambi na wenzake walisikia kishindo juu ya paa la choo cha nje na wakaona moto ukiwaka huku pembeni yake kukiwa na dumu lenye mafuta ya petroli ndipo wakanza kuzima moto huo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger