"Wanaume wa Mbeya wanapenda kulelewa"- Chalamila

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa mkoa wa Mbeya, wameachiwa jukumu la kuendesha familia zao huku wanaume wakiongoza kufanya vitendo vya dhuluma dhidi ya mali zinazotafutwa na wake zao.


Chalamila ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la sita la jinsia ngazi ya wilaya, ambalo limefanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.


RC Chalamila amesema kuwa wanawake wengi mkoani humo, ndiyo wanaobeba majukumu ya kutunza na kulea familia, ambapo hufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo kuuza mboga na matunda, wakati wanaume wakitumia mwanya huo kuwafanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni  pamoja na kunyang'anya fedha wanazopata kwenye biashara na kwenda kuhonga michepuko.

"Idadi kubwa ya wanaume mkoani Mbeya, wanapenda kulelewa hawapendi kujishughulisha, wanawategemea wanawake kulisha familia na kufanya kila kitu, mbaya zaidi huwashinikiza wake zao kuomba mkopo kwa kutumia account zao ili wadhulumu hizo hela, nawaambia wanawake msikubali kutumika kama ndoa yako ina shida  ondoka kaanzishe maisha mengine", amesema RC Chalamila.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndiyo Marioo's hasa Msanii , Utamzalishaje Faiza alafu umwachie majukumu ya Malezi aende kusukuma matoroli Bangi Coooki tailandi.

    inakuaje akutumie pesa ww unatanua.

    Asante RC, Washughulikie hawa Marioos.

    ReplyDelete

Top Post Ad