Wanigeria Waikazia SIMBA, Figisu Mwanzo MwishoIKIWA leo Novemba 29 Simba wanashuka Uwanja wa New Jos kusaka ushindi mbele ya wapinzani wao Plateau Unted kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika mambo yamezidi kuwa magumu kwa wapinzani hao kuendelea kufanya mipango ya kuwatoa mchezoni Simba.


Kazi kubwa leo itakuwa kwenye kusaka ushindi ndani ya uwanja na ikiwa wawakilishi wa Tanzania Simba hawatakuwa makini basi wanaweza kupoteza mchezo wa leo kutokana na mambo ambayo wamekutana nayo.


Awali baada ya kufika  mji wa Jos ambapo ndipo ipo kambi ya wapinzani wao Plateau United ilielezwa kuwa wachezaji na viongozi wa Simba waligomewa kutumia wapishi wao maalumu jambo lililoanza kuwavuruga mwanzo.


Pia kabla ya mchezo kuchezwa inaelezwa kuwa kulikuwa na mpango wa kuwatoa wachezaji muhimu kikosini ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Luis Miquisssone, John Bocco na Jonas Mkude kwa kutaka waonekane na Virusi vya Corona ili wasicheze mchezo wa leo.


Pia wapinzani hao ambao waliwahi kuingia kwenye kashfa ya kupanga matokeo ndani ya Nigeria wamegomea mchezo kuonyeshwa mubashara.


Kupitia kwa Mtendaji Mkuu wa Simba, (CEO) Barbara Gonzalez amesema:- “Plateau United wamekataa kuruhusu mechi kurushwa mubashara. Licha ya juhudi zetu zote tukishirikiana na mshiriki wetu AZAM TV, mwenyeji wetu amekataa kushirikiana kwenye hilo.


"Nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa wapenzi wetu wote ulimwenguni ambao walitaka kuangalia mechi hii. Mpaka muda huu, tunapigania hii mechi iweze kuoneshwa mubashara (live).” 


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments