Warembo 20 wa Miss Tanzania kuingia kambini Novemba 26

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Warembo 20 kutoka Kanda 5  za mikoa ya Tanzania wanatarajia kuanza kambi ya mchuano wa Fainali za Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tarehe 26 Novemba 2020 jijini D’salaam. 

Hatua za awali za mashindano haya ulianza mapema mwezi Februari mwaka huu, baadae mchakato ulisitishwa kidogo kutokana na janga la ugonjwa wa Corona ulioikumba nchi yetu pamoja na dunia kwa ujumla. 


Mchakato wa kuwapata washiriki 100 wa awali uliendelea mwezi Juni mara baada ya tishio la ugonjwa wa virus vya Corona kumalizika, ambapo mchujo wa washiriki 100 ulifanyika na kuwapunguza hadi washiriki 50. 


Washiriki 50 walipewa majukumu ya kufanya  na kuwasilisha majibu yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania ambao ndio walikuwa na jukumu la kudadisi na kuperuzi  majibu ya washiriki wote. 


Kati ya washiriki 50 ni washiriki 20 tu ndio waliopita katika mchakato huo, nao wameshajulishwa tayari kuhusu kuingia kambi ya Miss Tanzania mwisho wa mwezi Novemba. 


Majina ya washiriki hao pamoja na umri wao ni  kama ifuatavyo:-




1. PRISCA LYIMO  umri miaka 22




2. TAMIA HAKAM  miaka 19




3. JULIANA RUGUMISA miaka 23




4. REHEMA CUTHBERT miaka 21




5. YVONNE PAUL miaka 20




6. RUTH BENITHO miaka 23 




7. GRACE MACHIBULA miaka 24




8. ROSE MANFERE miaka 20




9. MARGARET MWAMBI miaka 23




10. SARAFINA MAGEYE miaka 20




11. MARTHA GOLODI miaka 23




12. ZENITHA CHUNDU miaka 22




13. DEOLYN MOLLEL miaka 21




14. HOYCE BAKANOBA miaka 20




15. NECERIAN KIVUYO miaka 20




16. RAZIA ABRAHAM miaka 19




17. ANGELA PENDAELI miaka 23




18. ADVERA MWEMBA miaka 21




19. VERYNICE DEOKARI miaka 24




20. GLORIA FELA miaka 23




Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania yanaandaliwa na Kampuni ya The Look chini ya Mkurugenzi wake Bi. Basilla Mwanukuzi Shayo. Miss Tanzania 1998. 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad