11/07/2020

Watoto 11 Wakamatwa kwa Kuiba Nyumbani kwa AskariJeshi la Polisi mkoa wa Tabora linawashikilia watoto 11, ambao ni wanafunzi wa shule za msingi kwa tuhuma mbalimbali za uvunjaji, uporaji na unyang’anyi wa kutumia nguvu na silaha katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Tabora mjini na kwamba walivunja nyumba ya Askari mstaafu na kuiba.


Kauli hiyo imetolewa hii leo Novemba 6, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Barnabas Mwakalukwa, na kusema kuwa watoto hao ni wenye kati ya miaka 10 hadi 14.


"Hawa watoto walivunja nyumba ya Askari mstaafu na kuiba, Laptop 1, simu 1 na Solar pannel, walipohojiwa walikiri kuhusika na matukio ya wizi, tunaendelea kuwahoji ili tupate mtandao wao wote na kumaliza kabisa hili tatizo ambalo kwa sasa hapa Tabora limeanza kuibuka tena", amesema ACP Mwakalukwa.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger