Watu 7 Mbaroni Kwa Kuhujumu Miundo Mbinu ya ReliJeshi la Polisi #Tanzania limewafikisha Mahakama ya Kibaha Watu saba wakituhumiwa Kuhujumu Uchumi kwa kukutwa wakisafirisha vyuma chakavu vikiwemo vyuma vilivyoibiwa kwenye Reli

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Richard Boaz amesema, miongoni mwa Watuhumiwa waliofikishwa Mahakamani ni pamoja na Mawakala na Wafanyabiashara wenye Viwanda vya Kuchakata Vyuma Chakavu

Boaz amesema, Serikali inatumia fedha nyingi kuimarisha miundombinu ikiwemo ya Reli lakini baadhi ya watu wasio wema na wenye uchu wa mali wamekuwa wakihujumu jitihada hizo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments