Wizi wa Mafuta, Ewura Yawataka Wenye Magari Kuwa Makini....

 


Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo, amewataka wanaokwenda kujaza mafuta kuhakikisha pampu inasomeka alama 00 ndipo waanze kujaziwa mafuta, vinginevyo wanaweza kuibiwa.


Ili kuepuka usumbufu, wenye Magari wanashauriwa kuachana na tabia ya kubaki kwenye magari wakiendelea na mambo mengine kwa kuwa hali hiyo inatoa mwanya wa kuibiwa


Ameongeza kuwa, Wakala wa Vipimo (WMA), imekuwa ikifanya ukaguzi wa pampu za Vituo mara kwa mara kuhakikisha watumiaji hawaibiwi, lakini wanunuzi wa mafuta nao wanapaswa kuwa waangalifu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments