Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Yanga Yaambulia Sare Kwa Gwambina

 


Kocha mkuu wa Yanga raia wa Burundi Cedric Kaze raia wa Burundi inaonekana kama ameelekeza nguvu zake zaidi katika mchezo ujao dhidi ya Simba SC, hiyo ni baada ya mchezo wa leo dhidi ya Gwambina kufanya mabadiliko makubwa.


Kaze asilimia 70 ya kikosi kilichocheza dhidi ya Gwambina na kulazimishwa sare 0-0 ugenini kilikuwa na maingizo mapya, huku wachezaji wake wa kikosi cha kwanza wengi kutowaweka hata benchi ikiwemo nahodha wao Lamine Moro.


Baadhi ya wachezaji wa Yanga waliokuwa wamepumzishwa ni Haruna Niyonzima, Feisal Salum, Lamine Moro, Adeyun Salehe, mchezo wa leo ambao Yanga wamepoteza point kwa Gwambina ambao hawako vizuri Ligi Kuu.


Yanga wameishia kupiga mashuti mawili tu On Target huku Gwambina wakipiga matatu, Yanga waliishia kuutawala mchezo kwa asilimia 54 kwa 46, sasa Yanga wanaenda kucheza Derby dhidi ya Simba SC November 7 2020.


 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments