Yanga Yaichapa JKT Taifa, Wazidi Kupaa KileleniTimu ya Yanga leo Novemba 28 imefanikiwa kuondoka na pointi zote tatu kwenye Uwanja wa Mkapa  jijini Dar, baada ya kuifunga JKT Tanzania ya Dodoma kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

 

Goli pekee la timu ya Wananchi limewekwa Nyavuni na Deus Kaseke ambaye amefunga mabao mawili kwenye mechi mbili mfulululizo akiwatungua Azam na leo akiwaadhibu JKT.

  

Licha ya kumkosa Nahodha wao Lamine Moro bado Yanga wameendelea kuwa ukuta ngumu kufungika, japokuwa safu ya ushambuliaji inaonekana kukosa makali ya kufamania nyavu hii ikiwa ni mwendelezo wa kushinda magoli yasiozidi mawili.

Kwa ushindi huo kiduchu Yanga imezidi kujikita Kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 31.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments