Yanga Yaukomalia Ubingwa wa Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KIUNGO mzawa Feisal Salum, ameweka bayana kuwa wamekubaliana kupambana msimu wa 2020/21 kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 24, imefunga jumla ya mabao 12, kinara ni Azam FC mwenye pointi 25 na watani zao wa jadi Simba wamejenga ngome nafasi ya tatu na pointi 20, zote zimecheza mechi 10.


 


Kwa misimu mitatu mfululizo, Yanga imewashuhudia watani zake wa jadi Simba wakitwaa taji la ligi kuanzia msimu wa 2017/18, 2018/19 na 2019/20. Ndani ya Yanga, Fei Toto ambaye amecheza jumla ya mechi tisa na kuyeyusha dakika 779 uwanjani, ni miongoni mwa viungo bora kwa msimu wa 2020/21.


 


Kiungo huyo amesema: “Tunajua kwamba hatujachukua ubingwa miaka mitatu mfululizo, kwa sasa kazi imeanza, ninaamini kwamba tutafi kia malengo ya kutwaa ubingwa na kurejesha furaha kwa mashabiki.” Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, ameliambia Championi Ijumaa kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuweza kutwaa ubingwa msimu huu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad