Yusuph Mhilu: Tumeanza Kujenga Hali ya KujiaminiYUSUPH Mhilu mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Kagera Sugar kinachonolewa na Kocha Mkuu, Meck Mexime amesema kuwa taratibu wachezaji wanaanza kujenga hali ya kujiamini jambo linalowapa nafasi ya kupata matokeo.

 

Mhilu kibindoni ametupia jumla ya mabao manne kati ya 11 ambayo yamefungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya 12 na pointi zake 14 kibindoni.

 

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa mwanzo mambo yalikuwa magumu kutokana na wachezaji kutengeneza muunganiko ambao umeanza kupatikana.

 

“Awali ilikuwa ngumu kupata matokeo kutokana na wachezaji kupambana kutengeneza muunganiko wa timu hasa ukizingatia kwamba ushindani ndani ya ligi ni mkubwa.

 

“Kwa sasa tumeanza kurejea kwenye ubora taratibu kutokana na mbinu ambazo tunapewa hivyo bado imani yetu ni kuendelea kusaka matokeo chanya ndani ya uwanja hivyo mashabiki watupe sapoti,” amesema.

 

Ihefu FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 18 na pointi zake sita bada ya kucheza mechi 12, kinara ni Yanga mwenye pointi 28 baada ya kucheza mechi 12.

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments