Zitambue Faida 7 za kuwa na Ratiba Binafsi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Ratiba siyo muhimu tu kwa ajili ya taasisi fulani pekee; ni muhimu pia kwa mtu binafsi. Watu wengi hushindwa kutumia muda wao vyema kutokana na kutokuwa na ratiba nzuri inayoeleweka. 


Kuweka ratiba kutakuwezesha kupangilia kazi na mipango yako kwa namna ambayo utaweza kuitekeleza vyema. 


Ikiwa unataka kuwa mwenye tija na ufanisi zaidi, basi fahamu faida 7 za kuwa na ratiba binafsi. 


1. Kutumia muda vyema 

Moja kati ya manufaa makubwa ya kuwa na ratiba ni kuweza kutumia muda vyema. Unapokuwa na ratiba ni vigumu kupata muda ambao haujapangiwa jukumu au kazi kwenye ratiba. 


Unapokuwa na ratiba muda wako wote utatumika vizuri tena kwa shughuli yenye tija iliyopangwa. Hivyo ni vyema kuhakikisha unajiwekea ratiba na unaifuata ipasavyo. 


2. Kuweka vipaumbele 

Kuweka ratiba ni mbinu mojawapo ya kuweka vipaumbele. Unapoweka ratiba ni lazima utaondoa mambo yasiyo ya msingi ili ratiba yako ikae vyema na itekelezeke. 


Kwa kujiwekea ratiba nzuri utaondoa mambo ambayo kimsingi hayakuwezeshi kufikia malengo yako. Kwa mfano huwezi kuweka muda wa kuchat kwenye ratiba. 


3. Kuongeza ufanisi 

Kufanya vitu bila mwongozo au mpangilio hukufanya ukose ufanisi. Kwa kuwa na ratiba utaweza kuwa na kitu kinachokuongoza na kukupa mpangilio mzuri. 


Mara siku inapoanza unakuwa tayari umeshafahamu unaaza na nini na kinafuata nini badala ya kushika hiki na kile. 


4. Kutokusahau mambo 

Ni vigumu sana kusahau jambo ambalo lipo kwenye ratiba yako. Hii ni kutokana na sababu kuwa unafanya kazi kwa kufuata ratiba, kila mara utakuwa unatazama ratiba yako inataka ufanye nini na kwa muda gani. 


Unaposahau mambo unayotakiwa kuyafanya, unapaswa kurejea kwenye ratiba yako na kutazama inataka ufanye nini. 


5. Kupata muda wa kupumzika 

Watu wengi wanakosa muda wa kupumzika kwa sababu wanafanya hiki mara kile bila mpangilio maalumu. Hili huwafanya kuhangaika siku nzima bila hata kujua wamekamilisha nini. 


Utamsikia mtu akisema “leo nimechoka sana hata sijui nimefanya nini” “leo nahangaika tu hata hamna nilichofanya”. Hii inaonyesha kuwa mtu huyu amechoka bila hata kukamilisha kazi zake. 


Kwa kujiwekea ratiba utaweza kupanga muda wa kazi na muda utakaoutumia kwa ajili ya kupumzika. 


6. Utaweza kuacha tabia mbaya 

Mbinu mojawapo nzuri ya kuacha tabia mbaya ni kujipangia ratiba ngumu na kuifuata. Kama kuna muda ambao unautumia kufanya matendo kamavile ulevi, matumizi ya madawa ya kulevya, uzinzi, umbea, n.k. Basi upangie muda huo majukumu mengi kwenye ratiba yako. 


Kwa kuzingatia hili hutopata muda wa kupoteza kufanya matendo au tabia ambazo kimsingi siyo nzuri. 


7. Unapata utulivu wa akili 

Mtu unapokuwa unafanya kazi bila mpangilio ni rahisi kukosa utulivu wa akili kwani mara utasahau jambo muhimu au utafanya mambo nje ya wakati. 


Ikiwa umeajiriwa unaweza kukosana na mwajiri wako kwa kuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yako vyema. Jambo hili linaweza kukunyima utulivu wa kiakili. 


Lakini ukiwa na ratiba utafanya mambo kwa mpangilio huku ukiwa umetulia kabisa bila tatizo lolote akilini mwako. 


Hitimisho 


Kwa hakika hatuwezi kufanya mambo yafanikiwe na kwa wakati ikiwa hatutakuwa na ratiba nzuri tunayoifuata kikamilifu. Ni muhimu ukatenga muda ukaanda ratiba yako ya siku, wiki au hata mwezi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad