Abdu Kiba afunguka sakata la Mke wa Alikiba

 
Mdogo wa msanii Alikiba kutoka Kings Music Records,  Abdu Kiba amevunja ukimya kwa kile kinachoendelea mitandaoni kuhusu video ya Nandy na Alikiba kwamba imesababisha sintofahamu kwenye ndoa ya kaka yake huyo na shemeji yake Aileenalora.


Akijibu kuhusiana na hilo baada ya kusambaa kwa maneno kuhusu matendo ya video hizo za nyuma ya kamera katika wimbo wa nibakishie ya Nandy ft Alikiba, Abdukiba amesema kuwa 


"Siwezi kujibu suala la Ali na mke wake kwa sababu silali nao hivyo sijajua kuna nini, ila kwenye familia hakuna tatizo kwa sababu wanajua sisi ni wanamuziki pia tushapata idhini kutoka kwa Mama ingawa kunaonekana na kuhisiwa kuna matendo tofauti, kazi za mitandaoni hatuwezi kuzijaji na huwezi kumpangia mtu akujibu nini" amejibu Abdu Kiba 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments