Alikiba Kwenye Mtihani Mzito
DAR: Mfalme wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, anadaiwa kuwa kwenye mtihani mzito, Gazeti la IJUMAA limedokezwa.

 

Imefahamika kwamba, Kiba yupo kwenye shinikizo kutoka kwa mashabiki wake la kumtaka kutimiza ahadi yake ya kuachia ngoma tatu kwa mpigo kabla mwaka huu wa 2020 haujageuka. Usisahau, leo zimebaki siku 20 tu mwaka huu umalizike.

 

Kila Kiba akifanya jambo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, mashabiki wake wamekuwa na jambo lao hilo wakimshinikiza kuachia nyimbo hizo kwani tayari wameanza kummisi baada ya wimbo wake wa mwisho wa Mediocre.

 

Kwa jumla kuna kitu mashabiki wake wanakisubiria kukisikia au kukiona kikifanywa na Kiba kama alivyowaahidi.
“Usijisahaulishe Officialalikiba tuna jambo letu kabla mwaka haujaisha.
“Tunaona siku zinayoyoma, halafu tunaona kimya.

“Tunakukumbusha lile jambo letu ni lini?
“Mfalme achia hayo madude tuwanyamazishe upande wa pili…” Ilisomeka sehemu ya maoni lukuki kwenye ukurasa wa Kiba wa Instagram baada ya kuposti video ikimuonesha akiwa studio akipiga kinanda.

 

Baada ya ngoma yake ya Mediocre iliyotikisa vilivyo, kabla ya mwaka huu kugeuka, Kiba aliahidi kuachia ngoma tatu na kuna bonge la kolabo ya wimbo mwingine mkali unaokwenda kwa jina la Nakupenda. Wimbo huo amefanya na DJ maarufu wa nchini Afrika Kusini aitwaye DJ SBU.

Stori: Khadija Bakari


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments