Aunty Ezekiel Awajia Juu Wanaofatilia Maisha Yake Hasa Wanaotaka Kujua Baba wa Mtoto Wake

 


 Staa wa filamu hapa nchini @auntyezekiel ambaye pia ni mama wa watoto wawili kwa sasa, awajia juu wale wote wanaofuatilia hasa maisha yake juu ya baba mtoto wake wa pili.


#Aunty alijifungua mtoto wake huyo wa pili, #Noman, Novemba 17, 2020 huku kukiwa na shauku kwa mashabiki zake kutaka kujua nani baba wakichanga hicho, ambapo bado likibaki kuwa fumbo kubwa kwani mara zote staa huyo amekuwa akikwepa kumtaja.


Sasa Leo kupitia ukurasa wake wa #Instagram, ameweka wazi kukasirishwa na baadhi ya mambo yanayoendelea mtandaoni kuhusu mtu aliyezaa naye mtoto huyo, kufikia hatua ya kuvalishwa mababa wasiohusika.


"Ni mtoto wangu mimi kazaliwa na baba gani Mweupe,mweuzi wa blue hayo hayawahusu jamani naomba nimeseme kitu kimoja katika maisha haukuna anayepangiwa maisha hakuna afundishwaye cha kufanya kama nyie ni wajuzi wa haya nifundisheni na kuoata hela za kula basi...."


"Point ni hii SITAKI SITAKI SITAKI kutungiwa baba wa mtoto wangu awe kijana awe mzee hayo ni maisha yangu binafsi maana hata nikizaa na nani hakuna atakaye nisaidia hela ya kuwalea hawa wananchi nikazi yangu mimi mwenyewe binafsi hivyo basi msimwekee mwanangu mababa wasio husika, Asante," alimalizia @auntyezekiel

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments