Bangi Haina Madhara...UN Wapiga Kura Kuhalalisha Matumizi ya Bangi

 


TUME ya Umoja wa mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya, imepiga kura na kupitisha pendekezo la Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kuondoa bangi katika orodha ya kundi la dawa hatari zaidi ambapo hatua hiyo huenda  ikachochea uzalishaji wa mmea huo kwa matumizi ya kimatibabu.

 

Kati ya nchi 53 wanachama, nchi 27 zilipiga kura ya kuunga mkono mapendekezo hayo huku nchi 25 zikipinga na Ukraine haikupiga  kura hiyo.  Miongoni mwa mataifa yaliyopiga kura ya kuunga mkono mapendekezo hayo, ni pamoja na Marekani na nchi za Ulaya huku China, Misri, Nigeria, Pakistan na Urusi zikiwa miongoni mwa nchi zilizopinga kuhalalisha mmea huo.

 

Hatua hiyo ya kihistoria inatarajiwa kufungua milango kwa mmea huo wa bangi kutambulika kwa manufaa yake kama dawa na tiba na pia itakuwa rahisi kwa nchi kufanya utafiti.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments