Biden Ateua Mmarekani Mweusi Kuwa Waziri wa Ulinzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



RAIS mteule wa Mararekan,i Joe Biden,  amemteua Jenerali Mstaafu, Lloyd Austin, kuwa waziri wake wa ulinzi, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.

 

Iwapo ataidhinishwa, Austin mwenye umri wa miaka 67-ambaye alistaafu mwaka 2016, atakuwa Mmarekani wa kwanza mweusi kuwahi kuiongoza Pentagon.   Austin anasubiri kuthibitishwa na bunge.

 

Biden amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa  jamii za Wademoctrat Weusi, Waasia na Walatino wakimtaka kuteua watu kutoka jamii hizo, kuchukua nyadhifa za uwaziri.

 

Jenerali Austin alihudumu chini ya utawala wa Obama, akiongoza kituo kikuu cha Marekani kinachotoa amri kuu za kijeshi, ambacho wajibu wake ulikuwa ni pamoja ni kutoa miongozo kuhusu Mashariki ya Kati na Asia kati ya mwaka 2013 na 2016.

 

Alishiriki pia kwenye kupanga mashambulio dhidi ya kundi la Islamic State katika nchi za Iraq na Syria.

 

Kabla ya hapo alikuwa naibu mkuu wa majeshi, na jenerali wa mwisho wa vikosi vya majeshi ya Marekani nchini Iraq.  Katika miaka hii alifanya kazi kwa karibu na Biden, ambaye alikuwa ni makamu wa rais katika utawala wa Obama.

 

Austin ana sifa ya uongozi bora na mchapa kazi, kutoa mahojiano kidogo kwa waandishi wa habari na kuchagua kukutoongea wazi kuhusu harakati za kijeshi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad