Bocco na Mkwasa Waibuka Washindi VPL Novemba

 


Bodi ya ligi imemtangaza nahodha wa Simba SC John Bocco kuwa mchezaji bora wa mwezi wa Novemba wa ligi kuu soka Tanzania bara na kocha wa klabu ya Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa kuwa kocha bora wa mwezi novemba baada ya wawili hao kuzisaidia timu zao kufanya vizuri kwenye VPL.

 

Kamati ya tuzo hizo zinazohusisha baadhi ya makocha imefanya uchambuzi na kumchagua Bocco kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba baada ya mshambuliaji huyo kuwapiku Mshambuliaji wa Ruvu Shooting Abdulrahman Mussa na kiungo wa Yanga Deus Kaseke alioingia nao fainali.

 

Kwa Upande wa kocha, tuzo hiyo imeenda kwa kocha wa Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa baada ya kuwagaragaza kocha wa Gwambina Fulgence Novatus na Mecky Mexime wa Kagera Sukari baada ya kuiongoza Ruvu kuvuna alama nyingi kuliko klabu nyingine yeyote kwenye VPL.


Mkwasa amevuna alama 11 baada ya kuiongoza Ruvu kupata ushindi michezo mitatu na sare mbili na matokeo hayo kuisaidia klabu hiyo kutoka nafasi ya 10 na kupanda hadi nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.  

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments