Boko Haram Yadai Kuwateka Nyara Mamia ya Wanafunzi NigeriaWaziri wa ulinzi wa Nigeria Ikuna Bakori amesema serikali itafanya kila liwezekanalo kuwaokoa mamia ya wanafunzi wa kiume waliotekwa nyara na watu waliokuwa na silaha katika eneo la Katsina. 

Akizungumza na DW, Bi Bakori amesema kuwa amesikitishwa sana na tukio hilo. Mtoto wake mwenye umri wa miaka 14, Ahmed Bakori ni miongoni mwa wavulana waliochukuliwa mateka kutoka shule ya sekondari ya serikali Ijumaa usiku. 


Gavana wa wa jimbo la Katsina, la kaskazini magharibi mwa Nigeria, Aminu Bello Masari amesema idadi ya wavulana wasiojulikana waliko ni 333, lakini mamlaka za shule zimesema wanafunzi 668 katika sajili yao bado hawajulikani walipo. 


Kundi la wanamgambo wa itikadi kali Boko Haram limedai kuhusika na utekaji nyara. Kiongozi wao Abubakar Shekau, ameyasema hayo kwenye mkanda wa sauti ijapokuwa ni vigumu kuithibitisha sauti hiyo

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments