RAIS John Magufuli, leo Desemba 28, 2020 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Revocatus Kuuli.
Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Magufuli ametengua uteuzi wa Kuuli kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kutwaliwa kwa ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji usioridhisha na matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Philemon Sengati, kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja
Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:
DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE
0 Comments