Burna Boy Katika Tuhuma za Kumsaliti Mpenzi Wake Stefflon Don Kwa Mwanamitindo wa Nigeria


Nyota wa muziki Nigeria, msanii #BurnaBoy anatajwa kumsaliti mpenzi wake, #StefflonDon kwa kutoka kimapenzi na mrembo aitwaye #JoPearl. Mrembo Jo Pearl aanika hilo.


#JoPearl kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameeleza kuwa aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na #BurnaBoy kwa miaka miwili. Kipindi ambacho pia #Burna yupo kwenye uhusiano na Stefflon Don.

#JoPearl amesema uhusiano wao ulianzia DM na baadaye kupelekea kuonana uso kwa uso nchini Uingereza.

#JoPearl ambaye ni mwanamitindo wa Nigeria na mfanyabiashara, katika kipindi chote cha mahusiano yao, anasema hakuwahi kulisikia jina la #StefflonDon toka kwenye kinywa cha Burna Boy.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments