Carlinhos Afanyiwa Vipimo Yanga SCKUFUATIA kusumbuliwa na mejeraha ya nyonga kwa muda mrefu, Kiungo wa Yanga, Carlos Carlinhos amefanyiwa kipimo cha MRI ili kubaini tatizo lake, huku akiendelea na matibabu zaidi.

 

Kabla ya kuumia nyonga, kiungo huyo aliyejiunga na Yanga msimu huu alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya kisigino yaliyomlazimu kukaa nje kwa muda mrefu akikosa mechi sita za Ligi Kuu Bara.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija, amesema: “Wachezaji wote wanaendelea vema isipokuwa Carlinhos, yeye anasumbuliwa na nyonga ambayo anaendelea nayo na matibabu.“

Kuanza mazoezi inategemea na uponaji wake, lakini kwa sasa tumempeleka kupima kipimo cha MRI ili kujua maendeleo yake.”

STORI: KHADIJA MNGWAI, Dar es Salaam


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments