Carlinhos Hatarini Kukosa Michezo Yote Yanga 2020

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





NYOTA wa Yanga, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ yupo hatarini kukosa michezo yote mitatu iliyosalia ya raundi ya kwanza kutokana na majeraha ya nyonga aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Namungo.

Carlinhos mwenye mabao mawili, hapo awali alikuwa akisumbuliwa na jeraha la kisigino lililomfanya akose michezo mitano alirejea na kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Namungo Novemba 22, mwaka huu.

 

Baada ya kupona majeraha hayo, Carlinhos amepata majeraha ya nyonga ambayo yamemfanya akose michezo mitatu mfululizo dhidi ya Azam, JKT Tanzania na mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting.



Akizungumza na Championi Jumatano,Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija alisema: “Ni kweli mchezaji wetu, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ anaendelea na matibabu baada ya hivi karibuni kufanyiwa tena vipimo vya afya ambavyo vimeonyesha wazi bado afya yake haijatengemaa na ataendelea kuwa kwenye uangalizi wa madaktari.

 

“Mpaka sasa hatuna uhakika wa muda rasmi ambao atakuwa nje ya uwanja kwa sababu hii itategemea sana na kasi ya uponaji wa majeraha aliyonayo, lakini kuna uwezekano mkubwa akakosekana kwenye michezo mitatu iliyosalia ya mzunguko wa kwanza,” alisema Mngazija.

Stori na Joel Thomas, Dar es Salaam | Championi Jumatano

L
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad