Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

CAS Yampiga Stop Morrison, Yanga Wachekelea

 


KIMENUKA! Ndivyo utakavyoweza kusema baada ya Mahakama ya Usuluhishi ya Masuala ya Soka ya Kimataifa (CAS) kumtumia barua ya kumsimamisha kiungo mshambuliaji wa Simba, Mghana, Bernard Morrison kucheza soka hadi pale kesi yake itakaposikilizwa upya na hukumu kutolewa.


 


Hiyo ni baada ya Yanga kupeleka mashitaka yao CAS ikiomba sakata hilo kusikilizwa upya baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumuamuru Morrison kuichezea Simba.


 


Kamati hiyo iliamuru Mghana huyo kuichezea Simba baada ya kubaini mkataba wake wa awali na Yanga kuonekana una mapungufu, maamuzi hayo yaliwafanya viongozi wa Yanga kukimbilia CAS kwenda kukata rufaa.


 
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka ndani ya Simba, CAS imemtumia barua kiungo huyo ikimtaka kutoendelea kuitumikia timu hiyo katika mashindano yoyote ikiwemo Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.


 


Mtoa taarifa huyo alisema zaidi ya wiki moja na nusu sasa zimepita tangu kiungo huyo mwenye mbwembwe za kuupandia mpira kupokea barua hiyo ya kumzuia kuichezea Simba hadi pale kesi hiyo itakaposikilizwa na hukumu kutolewa na CAS.


 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments