Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Chelsea na West Ham kitaeleweka leo EPL

Klabu ya Chelsea inataraji kujitupa dimbani kuvaana na wagonga nyundo wa jiji la London klabu ya Westham United kwenye mchezo wa EPL unaotazamiwa kupigwa saa 5 kamili usiku wa hii leo kwenye dimba lake la nyumbani la Stamford Bridge.
Kueleke kwenye mchezo huo Kocha wa Chelsea Frank Lampard huenda akawarejesha kikosini washambuliaji wake Hakim Ziyech na Callum Hodson Odoi baada ya nyota hao kupona majeraha yao na kufanya mazoezi ya pamoja na timu tokea ijumaa ya juma lililopita.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa wenye upinzani mkali pale ambapo Chelsea anahaha kusaka ushindi kwa hamu kubwa mara baada ya kupoteza michezo yake miwili mfululizo kwenye EPL na wakati huo huo Westham wakitaka kuendeleza wimbi la ushindi kwa kutokupoteza mchezo.

Kwa Upande wa Westham, Kocha wake David Moyes yupo njia panda baada ya kukosa jibu la moja kwa moja kama mshambuliaji wake Michael Antonio atakuwa fiti kuwavaa Chelsea baada ya nyota wake huyo kuwa nje  ya uwanja tokea mapema mwezi Novemba.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments